Hamia kwenye habari

Urusi

 

2022-02-08

URUSI

Mashahidi wa Yehova Katika Eneo la Irkutsk Wadumisha Uaminifu Licha ya Kuvamiwa kwa Ukatili Nyumbani

Oktoba 4, 2021, mfululizo wa uvamizi wa nyumba ulitukia katika eneo la Irkutsk. Wakati wa uvamizi huo Mashahidi wahojiwa na kupigwa kwa ukatili. Baada ya hapo, Mashahidi sita wa Yehova walipelekwa mahabusu kwa sababu tu ya kushiriki imani yao ya Kikristo kwa amani.