Hamia kwenye habari

Urusi

 

2018-05-21

URUSI

Mahakama ya Oryol Yasikiliza Ushahidi wa Kwanza wa Kesi ya Dennis Christensen

Bw. Christensen, amekuwa mahabusu tangu Mei 2017. Anaweza kukabili kifungo cha miaka sita hadi kumi gerezani kwa sababu tu ya kushiriki utendaji wake wa kidini.

2018-05-10

URUSI

Kampeni ya Kuwatisha Mashahidi wa Yehova Yaanza Nchini Urusi

Wenye mamlaka nchini Urusi wameyafungia mashirika ya kisheria ya Mashahidi wa Yehova, na sasa wameanza kuwashambulia Mashahidi na ibada yao.

2018-05-09

URUSI

Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wajaribu Kunyakua Mali Inayomilikiwa na Shirika la Mashahidi wa Yehova la Marekani

Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg itasikiliza rufaa ya Mashahidi wa Yehova kuhusu hukumu iliyotolewa ya kunyakua ofisi yao ya kitaifa nchini Urusi.

2018-01-12

URUSI

Rufaa Yakataliwa​—Mahakama ya Urusi Yaunga Mkono Uamuzi wa Kuitangaza Biblia Kuwa na “Msimamo Mkali”

Sasa ni kosa la jinai kwa mtu yoyote kuwasambazia wengine Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Hata tu kuwa na nakala ya Biblia hiyo kunaweza kumweka mtu kwenye hatari ya kutozwa faini kubwa au jambo lingine baya zaidi.

2018-01-04

URUSI

Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wachukua Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova

Uporaji huo umetukia juma moja baada ya uamuzi wa mahakama ambao unatishia kuchukuliwa kwa jengo lililotumiwa na Mashahidi wa Yehova kama makao yao makuu ya taifa, lililoko karibu na jiji la St. Petersburg.