Hamia kwenye habari

Urusi

 

2017-09-15

URUSI

Urusi Yaitangaza Biblia Kuwa na “Msimamo Mkali”

Mahakama ya Jiji la Vyborg iliitangaza Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya lugha ya Kirusi kuwa na ‘msimamo mkali,’ Biblia hiyo inachapishwa na Mashahidi wa Yehova katika lugha nyingi.

2017-10-02

URUSI

Maoni ya Mataifa Mbalimbali Kuhusu Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Mashirika mbalimbali ya kimataifa na maofisa mbalimbali wametoa maoni kuhusu uamuzi usio wa haki wa mahakama na serikali ya Urusi kushindwa kulinda uhuru wa ibada wa dini zenye waumini wachache.

2017-09-11

URUSI

Wajumbe wa Kimataifa Wawaunga Mkono Ndugu Zao Warusi Wakati wa Rufaa ya Mahakama Kuu

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova lilipanga wajumbe wasafiri kutoka mabara matatu hadi Moscow.

2017-08-14

URUSI

Mahakama Kuu ya Urusi Imehalalisha Hukumu Yake ya Awali ya Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova

Mahakama Kuu ya Urusi imekataa rufaa ya Mashahidi na kuthibitisha uamuzi wake wa Aprili 20. Mashahidi wa Yehova nchini Urusi watakata rufaa ili wapate haki katika ECHR na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu.

2017-07-09

URUSI

Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wawashukuru Mashahidi wa Yehova, Kutia Ndani Raia wa Denmark Aliyefungwa, kwa Utumishi Mzuri kwa Jamii

Maofisa jijini Oryol wawashukuru Mashahidi wa Yehova kwa utumishi wao kwa jamii. Kikundi hicho kilitia ndani Dennis Christensen, ambaye amefungwa hivi karibuni kwa kuhudhuria mkutano wa kidini wenye amani.

2017-07-09

URUSI

Video Inayoonyesha Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wakivamia Mkutano wa Kidini Wenye Amani

Video kwenye kituo fulani cha televisheni ilionyesha maofisa wa polisi wenye silaha na Usalama wa Taifa (FSB) wakivamia mkutano wa kidini wa Mashahidi wa Yehova huko Oryol, Urusi.

2017-07-09

URUSI

Video Inayoonyesha Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wakivamia Mkutano wa Amani wa Kidini

Mei 25, 2017, polisi wenye silaha na Usalama wa Taifa walivamia ibada ya Mashahidi wa Yehova huko Oryol, Urusi.

2017-07-21

URUSI

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Urusi Umekuwa na Matokeo Mabaya kwa Mashahidi wa Yehova

Uamuzi huo umewashushia heshima Mashahidi na umewapa baadhi ya watu na maofisa wa serikali ujasiri wa kuwatendea Mashahidi isivyofaa hata zaidi, kama mifano iliyoelezwa mwanzoni ambayo ilitokea karibuni.

2017-06-23

URUSI

Rais Putin Awapa Mashahidi wa Yehova Tuzo ya Mzazi Bora

Katika sherehe iliyofanywa huko Kremlin, Rais Vladimir Putin aliwapa Valeriy na Tatiana Novik tuzo ya “Mzazi Bora.” Wao ni Mashahidi wa Yehova wanaoishi Karelia.