Hamia kwenye habari

Ndugu Dennis Christensen akiwa kizimbani mwaka 2018

JULAI 8, 2020
URUSI

“Adhabu” ya Ndugu Christensen Yaongezwa kwa Siku Tano Baada ya Kusingiziwa Makosa Mengine

“Adhabu” ya Ndugu Christensen Yaongezwa kwa Siku Tano Baada ya Kusingiziwa Makosa Mengine

Julai 6, 2020, Ndugu Dennis Christensen alipaswa kutolewa kwenye jela ya adhabu. a Hata hivyo, siku hiyo, gereza la Lgov lilimwongezea siku nyingine tano, kwa kuwa walisema amevunja sheria nyingi za gereza, kama vile kuchelewa.

Ndugu Dennis Christensen alimwambia wakili wake kwamba wenye mamlaka wanasema uwongo ili kuhakikisha kwamba hataweza kupata msamaha na kuachiliwa mapema. Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, Ndugu Dennis Christensen alikuwa ametumikia sehemu kubwa ya kifungu chake cha miaka sita kumwezesha kuomba kuruhusiwa mapema. Ametuma ombi lake mara nne, lakini mahakama ya Lgov na maofisa wa gereza wamekuwa wakizuia ombi lake likubaliwe.

Wenye mamlaka nchini Urusi wameendelea kuwasingizia ndugu zetu wapendwa madai ya uwongo, lakini tunajua kwamba Yehova atawasaidia kwa kuwapa amani na ‘kuwazunguka kwa kibali kana kwamba kwa ngao kubwa.’—Zaburi 5:12; 119:69.

a Hivi karibuni tuliripoti kwamba muda mfupi baada ya mahakama kufanya uamuzi wa kumwachia huru Ndugu Dennis Christensen mapema, rufaa ilikatwa na Ndugu Dennis Christensen akafungiwa katika jela ya adhabu ya pekee iliyokusudiwa hasa wahalifu sugu (EPKT). EPKT ipo katika jengo moja pamoja na jela nyingine ya adhabu inayoitwa SHIZO, ambapo wafungwa waliofanya makosa madogo hufungiwa. Sasa imeeleweka kwamba alikuwa amefungiwa SHIZO.