Hamia kwenye habari

Ndugu Andrey Sazonov

AGOSTI 26, 2021
URUSI

Baba ya Watoto Wawili Anaweza Kufungwa Miaka 15 Gerezani kwa Sababu ya Imani Yake

Baba ya Watoto Wawili Anaweza Kufungwa Miaka 15 Gerezani kwa Sababu ya Imani Yake

Mfuatano wa Matukio

  1. Mahakama ya Jiji la Uray iliyo katika Eneo Lililotengwa la Khanty-Mansi—Yugra itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi ya Ndugu Andrey Sazonov. a Anaweza kufungwa miaka 15 gerezani

  2. Juni 22, 2020

    Kesi ya uhalifu ya Andrey yaanza

  3. Agosti 22, 2019

    Anaachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani lakini anawekewa vizuizi vya kusafiri na vizuizi vingine pia vilivyowekwa na mahakama

  4. Februari 26, 2019

    Anahamishiwa kifungo cha nyumbani

  5. Februari 6, 2019

    Azuiliwa kwa muda, kisha siku mbili baadaye anahamishiwa mahabusu baada ya mahali pake pa kazi na gari lake kufanyiwa msako

  6. Januari 31, 2019

    Anashtakwa kosa la uhalifu la “kutayarisha na kushiriki utendaji wa shirika lenye msimamo mkali”

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunathamini sana mfano mzuri ambao ndugu na dada zetu nchini Urusi wanaendelea kuweka wanapokabiliana na mateso. Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwafanya kuwa ‘jasiri na wenye nguvu.’—Zaburi 138:3.

a Tarehe ya hukumu haitolewi mapema pindi zote.