Hamia kwenye habari

Oktoba 2020, Dada Anna Lokhvitskaya akiwa nje ya mahakama

FEBRUARI 25, 2021
URUSI

Dada Anna Lokhvitskaya Anakabili Kifungo; Mume Wake, na Mama-Mkwe Wake Wameshtakiwa Pia

Dada Anna Lokhvitskaya Anakabili Kifungo; Mume Wake, na Mama-Mkwe Wake Wameshtakiwa Pia

HABARI ZA KARIBUNI | Mahakama ya Urusi Yamhukumu Dada Anna Lokhvitskaya

Julai 20, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan iliyo katika Eneo Lililotengewa Wayahudi ilimhumkumu Dada Anna Lokhvitskaya kifungo cha nje cha miaka miwili na nusu. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Hukumu Inatarajiwa

Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhan iliyo katika Eneo Lililotengewa Wayahudi itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayomhusu Dada Anna Lokhvitskaya. a Bado mwendesha-mashtaka hajatuma ombi la hukumu yake.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Anna Lokhvitskaya

  • Alizaliwa: 1993 (Birobidzhan)

  • Maisha Yake: Alilelewa na mama yake aliyemfundisha kutii viwango vya Biblia. Alibatizwa mwaka wa 2012. Ni stadi wa kushona nguo. Aliolewa na Artur, mwaka wa 2018. Wanapenda kuvua samaki, kusafiri na kucheza mpira wa wavu

Historia ya Kesi

Februari 6, 2020, Anna alikuwa miongoni mwa dada sita Wakristo walioshtakiwa na mamlaka za Urusi katika eneo la Birobidzhan kwa kushiriki katika utendaji “wenye msimamo mkali.” Jumla ya kesi 19 zilifunguliwa katika eneo hilo dhidi ya Mashahidi wa Yehova. Zinatia ndani kesi dhidi ya mume wa Anna, Artur, na dhidi ya mama-mkwe wake, Irina.

Kesi hizo za uhalifu zimewaletea changamoto nyingi wenzi hao wa ndoa vijana. Hawaruhusiwi kusafiri, hawawezi kuchukua pesa katika akaunti zao za benki, na hawaruhusiwi kutumia huduma zote za umma. Hali hiyo imemwathiri sana Anna kihisia hivi kwamba pindi nyingine amehitaji kutibiwa.

Anataja mambo kadhaa yanayomsaidia. Anasema hivi: “Njia moja inayonisaidia kukabiliana na hisia zangu ni nyimbo zinazopatikana katika JW Broadcasting. Nyimbo hizo hunituliza na kuwa na mtazamo unaofaa kuelekea hali mbalimbali ninazokabili. Kufanya mazoezi ya kimwili kumenisaidia kukazia fikira mawazo yanayofaa.”

Kwa kuongezea, Anna anasema kwamba yeye na Artur hujitahidi kutanguliza mahitaji ya wengine. Anasema hivi: “Tulijiwekea lengo la kuwapa wengine zawadi kila mwezi, hata ikiwa zawadi hizo ni ndogo. Tunajitahidi kuwafikiria wengine badala ya matatizo yetu tu.”

Akiwa anaendelea kusubiri hukumu yake, Anna anaona hali yake kuwa ‘nafasi nzuri ya kuonyesha ushikamanifu wake kwa Yehova kupitia matendo yake.’—Zaburi 18:25.

a Si pindi zote tarehe ya mapema ya hukumu inapotolewa