Hamia kwenye habari

Dada Viktoriya Verkhoturova

AGOSTI 18, 2021
URUSI

Dada Viktoriya Verkhoturova Anadumisha Shangwe Yake Licha ya Kukabili Kifungo

Dada Viktoriya Verkhoturova Anadumisha Shangwe Yake Licha ya Kukabili Kifungo

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 29, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Priokskiy iliyoko Nizhny Novgorod ilimhukumu Dada Viktoriya Verkhoturova kifungo cha nje cha miaka minne. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu

  2. Julai 17, 2020

    Viktoriya anawekewa vizuizi vya usafiri

  3. Machi 26, 2020

    Kesi ya uhalifu inafunguliwa dhidi ya Viktoriya

  4. Julai 17, 2019

    Maofisa kumi wa usalama, pamoja na mpelelezi wanaendesha upekuzi katika nyumba yake kwa saa tano. Walimweka Viktoriya katika chumba tofauti na mume wake, Sergey. Maofisa walijaribu kumtisha Viktoriya kwa kumwambia kuhusu hali mbaya zilizopo gerezani

Maelezo Mafupi Kumhusu

Licha ya mateso, ndugu na dada zetu nchini Urusi wanaendelea kuwa na shangwe kwa msaada wa Yehova. Tunajua ataendelea kuwaandalia ndugu hao wapendwa ‘shangwe na amani.’​—Waroma 15:13.