JULAI 10, 2023
URUSI
Dada Watatu Wahukumiwa Jijini Komsomolsk-on-Amur
Machi 23, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Centralniy iliyo Komsomolsk-on-Amur iliwahukumu Dada Tatyana Bondarenko, Dada Yelena Nesterova, na Dada Tatyana Svoboda kifungo cha nje cha miaka mitano kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwabariki na kuwaimarisha dada zetu wanapodumisha uaminifu chini ya majaribu.—Ruthu 2:12.
Mfuatano wa Matukio
Septemba 21, 2021
Kesi ya uhalifu yafunguliwa dhidi ya Tatyana Svoboda
Oktoba 18, 2021
Maofisa wa polisi waanza pia kuwapeleleza Tatyana Bondarenko na Yelena Nesterova
Oktoba 20, 2021
Nyumba zao zafanyiwa msako
Agosti 28, 2022
Mashtaka yafunguliwa
Desemba 28, 2022
Kesi ya uhalifu yaanza
Machi 23, 2023
Walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano kila mmoja