Hamia kwenye habari

ushoto kwenda kulia: Dada Kishta Tutinova, Dada Tsagan Khalgaeva, na Dada Yekaterina Menkova

JUNI 28, 2024
URUSI

Dada Watatu Wahukumiwa Katika Jamhuri ya Kalmykia, Nchini Urusi

Dada Watatu Wahukumiwa Katika Jamhuri ya Kalmykia, Nchini Urusi

Juni 24, 2024, Mahakama ya Jiji la Elista iliyo katika Jamhuri ya Kalmykia iliwahukumu Dada Tsagan Khalgaeva, Dada Yekaterina Menkova, na Dada Kishta Tutinova. Tsagan na Yekaterina walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili kila mmoja. Kishta alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunathamini sana mifano hiyo ya imani ya siku zetu. Na tunafurahi kujua kwamba Yehova anaona majaribu yote tunayokabili na atatuthawabisha kwa sababu ya uaminifu wetu.​—Zaburi 37:18.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 16, 2023

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Kishta

  2. Februari 28, 2023

    Nyumba ilifanyiwa msako. Kishta alipelekwa mahabusu

  3. Machi 1, 2023

    Tsagan alifukuzwa kazi kwa kuwa watu wengi walijua kwamba alifunguliwa kesi ya uhalifu. Kishta aliachiliwa kutoka mahabusu na akazuiliwa kutoka nyumbani

  4. Julai 21, 2023

    Kishta aliruhusiwa kutoka nyumbani

  5. Desemba 19, 2023

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Yekaterina na Tsagan. Wote wawili waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Februari 9, 2024

    Kishta aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  7. Aprili 1, 2024

    Kesi ya uhalifu ilianza

  8. Juni 24, 2024

    Hukumu ya kifungo cha nje ilitolewa