MACHI 6, 2024
URUSI
Dada Yelena Kozhevnikova Ahukumiwa Kifungo cha Nje cha Miaka Miwili
Machi 4, 2024, Mahakama ya Tsentralniy iliyo katika Wilaya ya Tolyatti Eneo la Samara ilimhukumu Dada Yelena Kozhevnikova. Alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunashangilia kujua kwamba Yehova anajibu sala zetu na kumpa Yelena “nguvu kupitia roho yake” pamoja na ndugu na dada wote wanaoendelea kuvumilia mateso.—Waefeso 3:16.
Mfuatano wa Matukio
Mei 15, 2023
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Mei 16, 2023
Nyumba ilifanyiwa msako
Mei 18, 2023
Aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Agosti 16, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza
Machi 4, 2024
Alihukumiwa miaka miwili ya kifungo cha nje
a Maelezo ya Dada Kozhevnikova yalichukuliwa kabla ya hukumu kutolewa.