Hamia kwenye habari

Kutoka kushoto hadi kulia: Ndugu Vladimir Melnik, Ndugu Vladimir Piskarev, na Ndugu Artur Putintsev

MEI 20, 2022
URUSI

Familia Zinavumilia Mateso Kwa Msaada wa Yehova

Familia Zinavumilia Mateso Kwa Msaada wa Yehova

Mahakama ya Wilaya ya Sovietskiy iliyo katika jiji la Oryol itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Vladimir Melnik, Ndugu Vladimir Piskarev, na Ndugu Artur Putintsev. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa hukumu anayopendekeza.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 8, 2020

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Ndugu Melnik, Ndugu Piskarev, na Ndugu Putintsev

  2. Desemba 9, 2020

    Maofisa wa usalama walipekua nyumba za familia nane za Mashahidi wa Yehova zilizo Oryol, kutia ndani nyumba za ndugu hao watatu. Ndugu hao watatu walipelekwa kizuizini

  3. Desemba 11, 2020

    Ndugu Melnik na Ndugu Piskarev walipelekwa mahabusu

  4. Desemba 14, 2020

    Ndugu Putintsev alipelekwa mahabusu

  5. Januari 19, 2021

    Wenye mamlaka walijulishwa kwamba Ndugu Piskarev alikuwa amezidiwa na ugonjwa lakini alikatazwa kumwona daktari na kupata matibabu

  6. Januari 21, 2021

    Ndugu Piskarev aliruhusiwa kutumia dawa alizoletewa na mke wake lakini bado alikatazwa kwenda hospitali

  7. Juni 24, 2021

    Ndugu Piskarev alichunguzwa kwenye hospitali na ikagunduliwa kwamba amepatwa na kiharusi. Licha ya hali yake mbaya ya afya alirudishwa mahabusu.

  8. Oktoba 29, 2021

    Mashtaka yalifunguliwa dhidi ya ndugu hao kwa kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  9. Januari 31, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Licha ya kwamba familia hizo zimetenganishwa kwa muda, tunafarijika kujua kwamba hakuna chochote ambacho kimewatenganisha na upendo wa Yehova na ulinzi wake.​—Waroma 8:38, 39.

a b c Kwa kuwa kwa sasa Ndugu Melnik, Ndugu Piskarev, na Ndugu Putintsev wako mahabusu, hatukuweza kupata maelezo kutoka kwao.