NOVEMBA 24, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: AGOSTI 21, 2023
URUSI
HABARI ZA HIVI KARIBUNI—NDUGU AFUNGWA | Tumeazimia Kuendelea Kumtumikia Yehova kwa Bidii Licha ya Mateso
Agosti 18, 2023, Mahakama ya Eneo ya Altai ilibadili hukumu ambayo Ndugu Pavel Kazadaev alikuwa amepewa awali ya kifungo cha nje na kumhukumu kifungo cha miaka mitatu gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.
Mei 29, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Industrialny District Court iliyo Barnaul katika Eneo la Altai ilimhukumu Ndugu Pavel Kazadaev kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Imani yetu inaimarishwa tunapowaona watu wa Yehova wakiendelea kumtumikia kwa bidii na shangwe licha ya majaribu.—Mathayo 5:11.
Mfuatano wa Matukio
Mei 11, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Mei 27, 2021
Maofisa wa polisi walianzisha msako ambao waliuita “Har-Magedoni.” Wakifanya msako huo, maofisa hao walipekua nyumba ya Pavel iliyo Novokuznetsk na pia nyumba ya watu wake wa ukoo wanaoishi katika eneo tofauti. Pavel na mke wake walipelekwa Barnaul, jiji lililo kilometa 350 kutoka nyumbani kwao, ili wakahojiwe. Pavel alishtakiwa kwa madai ya uhalifu, yaani, kwamba alishiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali, na akawekwa kizuizini
Mei 28, 2021
Aliachiliwa kutoka kizuizini na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Agosti 12, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza