Hamia kwenye habari

Ndugu Igor Gusev

NOVEMBA 15, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: NOVEMBA 17, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—APIGWA FAINI | Ametiwa Moyo na Wengine Wanaovumilia Mateso

HABARI ZA KARIBUNI—APIGWA FAINI | Ametiwa Moyo na Wengine Wanaovumilia Mateso

Novemba 17, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Zheleznodorozhny iliyo Krasnoyarsk ilimhukumu Ndugu Igor Gusev. Alipigwa faini ya rubo 600,000 (dola 9,907 za Marekani).

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 21, 2020

    Alikutana na wenye-mamlaka kwa mara ya kwanza walipomhoji kuhusu kesi inayomkabili Ndugu Vitaliy Sukhov

  2. Februari 17, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Igor kwa shtaka la kupanga utendaji wa shirika la kidini lililopigwa marufuku

  3. Agosti 23, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Sisi pia tunaimarishwa na kielelezo cha ujasiri ambao ndugu na dada zetu wanaonyesha. Kadiri tunavyoendelea “[kutafakari] matokeo ya mwenendo wao” tunachochewa “[kuiga] imani yao.”​—Waebrania 13:7.