Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Aleksandr Vasichkin, Ndugu Sergey Galyamin, Ndugu Anatoliy Lyamo, na Ndugu Vladimir Spivak

MEI 30, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: Machi 6, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—APIGWA FAINI | Ndugu Huko Teykovo Wakazia Fikira Msaada wa Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—APIGWA FAINI | Ndugu Huko Teykovo Wakazia Fikira Msaada wa Yehova

Februari 29, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Teykovskiy iliyo katika Eneo la Ivanovo iliwahukumu Ndugu Sergey Galyamin, Ndugu Anatoliy Lyamo, Ndugu Vladimir Spivak, na Ndugu Aleksandr Vasichkin. Kila ndugu alitozwa faini. Vladimir alitozwa faini ya rubo 600,000 (dola 6,564 za Marekani), Sergey alitozwa faini ya rubo 650,000 (dola 7,111 za Marekani) na Aleksandr na Anatoliy walitozwa faini ya rubo 1,100,000 kila mmoja (dola 12,034 za Marekani).

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunajua kwamba majaribu yoyote yale tutakayopata katika mfumo huu ni ya muda tu yakilinganishwa na baraka za milele ambazo Yehova amewawekea watumishi wake waaminifu.​—2 Wakorintho 4:17, 18.

Mfuatano wa Matukio

  1. Aprili 10, 2020

    Kesi ya uhalifu yafunguliwa

  2. Aprili 11, 2020

    Nyumba zafanyiwa msako

  3. Aprili 16, 2020

    Akina ndugu wawekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Februari 2, 2023

    Kesi ya uhalifu yaanza