FEBRUARI 21, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: MACHI 25, 2024
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | Aliimarishwa na Ndugu na Dada Wengi
Machi 22, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Tolyatti ilimhukumu Dada Yelena Yurenkova kifungo cha nje cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunamshukuru sana Yehova kwa kumtegemeza Yelena kwa upendo na wote wanaoendelea kuvumilia mateso huku tukiendelea ‘kumtumikia bega kwa bega.’—Sefania 3:9.
Mfuatano wa Matukio
Mei 15, 2023
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Mei 16, 2023
Nyumba ilifanyiwa msako. Akahojiwa na kuwekewa vizuizi vya kusafiri
Juni 5, 2023
Alifunguliwa mashtaka
Agosti 23, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza