Hamia kwenye habari

Dada Irina Perefileva

MEI 1, 2023| HABARI ZILIONGEZWA: AGOSTI 30, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | “Matatizo Yangu ni ya Muda Mfupi Tu”

HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | “Matatizo Yangu ni ya Muda Mfupi Tu”

Agosti 28, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Urupskiy iliyo katika Jamhuri ya Karachayevo-Circassian ilimhukumu Dada Irina Perefileva kifungo cha nje cha miaka mitano na miezi sita. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama vile Irina, sisi pia tunafarijika kujua kwamba hata majaribu yetu yawe magumu kadiri gani, ni ya ‘muda mfupi na ni mepesi’ yakilinganishwa na baraka ambazo Yehova amewawekea watumishi wake waaminifu.​—2 Wakorintho 4:17.

Mfuatano wa Matukio

  1. Januari 9, 2021

    Nyumba ilipigwa msako

  2. Novemba 22, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

  3. Novemba 23, 2021

    Nyumba ilipigwa msako tena

  4. Novemba 29, 2021

    Alihukumiwa kwa kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  5. Oktoba 15, 2022

    Aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Desemba 6, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza