DESEMBA 13, 2021 | HABARI ZILIONGEZWA: JUNI 13, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | “Shangwe Yangu Inatokana na Kuwa Karibu na Yehova”
Juni 6, 2023, Mahakama ya Jiji la Partizansk iliyo katika Eneo la Primorye ilimhukumu Dada Irina Buglak kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Mfuatano wa Matukio
Agosti 6, 2021
Kesi ya uhalifu dhidi ya Irina ilirudishwa kwenye Mahakama ya Jiji la Partizansk
Novemba 30, 2020
Kwa sababu hakukuwa na ushahidi, kesi ya Irina ilirudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka
Januari 31, 2020
Aachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani baada ya siku 107
Oktoba 16, 2019
Baada ya kuwekwa mahabusu kwa siku 179, Irina aliachiliwa na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani
Aprili 20, 2019
Maofisa wa FSB walifanya msako katika nyumba ya Irina saa tisa usiku. Wenye mamlaka walimshtaki kwa kupanga na kuongoza shughuli za kidini. Alipelekwa mahabusu na kifungo chake kiliongezwa mara tatu
Aprili 19, 2019
Maofisa nane wa FSB walivamia nyumba ya Dada Nelly Tarasyuk mwenye umri wa miaka 80. Irina na binti yake, Natalya, walikuwa miongoni mwa akina dada waliokuwa katika nyumba hiyo. Wakati wa uvamizi huo, Nelly akawa mgonjwa na kupelekwa hospitalini. Akina dada waliobaki walihojiwa usiku kucha. Irina alizuiliwa
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunasali kwamba Yehova aendelee kumwimarisha Irina, na pia, ndugu na dada zetu wapendwa nchini Urusi wanaoendelea kuvumilia kwa subira na shangwe.—Wakolosai 1:11.