Hamia kwenye habari

Dada Olga Zhelavskaya

JANUARI 17, 2023| HABARI ZILIONGEZWA: APRILI 17, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | “Yehova Yuko Karibu na Mimi Kila Wakati”

HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | “Yehova Yuko Karibu na Mimi Kila Wakati”

Aprili 17, 2023, Mahakama ya Metallurgicheskiy iliyo katika Wilaya ya Chelyabinsk ilimhukumu Dada Olga Zhelavskaya kifungo cha nje cha miaka miwili. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna uhakika kwamba hata tukikabili mateso ya aina gani, watumishi wa Yehova ‘hawatatikiswa kamwe’ kwa sababu anawategemeza kwa upendo.​—Zaburi 16:8.

Mfuatano wa Matukio

  1. Juni 16, 2018

    Wenye mamlaka waliweka vifaa vya kurekodi video na sauti katika nyumba ya Olga ili kufuatilia utendaji wake

  2. Machi 26, 2019

    Nyumba yake ilifanyiwa msako kwa sababu ya uchunguzi uliokuwa unafanywa katika kesi ya Ndugu Vladimir Suvorov

  3. Agosti 31, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa. Alishtakiwa kwa madai ya kuunga mkono utendaji wa shirika lenye msimamo mkali kwa kufanya mikutano ya shirika hilo nyumbani mwake

  4. Oktoba 22, 2021

    Alipatwa na ugonjwa wa kiharusi na kulazwa hospitalini

  5. Septemba 28, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza