Hamia kwenye habari

Kushoto: Dada Tatyana Galkevich; Kulia:Dada Valentina Vladimirova

JANUARI 24, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: FEBRUARI 16, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAHUKUMIWA | Dada Wawili Walio na Matatizo ya Afya Wamevumilia Hali Kizuizini Miezi Sita kwa Msaada wa Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAHUKUMIWA | Dada Wawili Walio na Matatizo ya Afya Wamevumilia Hali Kizuizini Miezi Sita kwa Msaada wa Yehova

Februari 14, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Promyshlenniy huko Smolensk iliwahukumu Dada Tatyana Galkevich na Valentina Vladimirova. Kila mmoja ahukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 14, 2019

    Wenye mamlaka walianzisha uchunguzi wa uhalifu dhidi ya Tatyana na Valentina. Polisi walifanya upekuzi katika nyumba za dada wote wawili, wakawazuilia, na kuwahoji kwa zaidi ya saa 48. Ingawa wote wawili wana matatizo mabaya sana ya afya, walipelekwa mahabusu

  2. Novemba 22, 2019

    Baada ya zaidi ya miezi sita, Tatyana na Valentina waliachiliwa kutoka mahabusu na kuhamishiwa kifungo cha nyumbani

  3. Desemba 31, 2019

    Valentina alipelekwa hospitali baada ya afya yake kuzorota

  4. Agosti 6, 2020

    Baada ya miezi minane, kifungo cha nyumbani cha Tatyana kiliondolewa na akaamriwa asiondoke eneo la nyumbani kwao. Valentina aliendelea kuwa chini ya kifungo cha nyumbani na aliruhusiwa kuwasiliana tu na wakili wake na mtu mmoja tu wa ukoo wa karibu

  5. Oktoba 2, 2020

    Wenye mamlaka waliwashtaki Tatyana na Valentina katika hati iliyokuwa na kurasa 400. Hati hiyo iliwashtaki dada hao kwa kupanga njama ya “kuficha utendaji wa shirika lenye msimamo mkali”

  6. Oktoba 14, 2020

    Kesi ilipoanza kusikilizwa, hakimu aliagiza kesi hiyo irudishwe kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka kwa sababu ilikuwa na ushahidi ambao haungeweza kutumiwa mahakamani. Ingawa Valentina hangeweza kusimama wakati wa kusikilizwa kwa kesi kwa sababu ya afya yake, mahakama ilikataa kuondoa kifungo chake cha nyumbani

  7. Februari 25, 2021

    Mahakama ya rufaa ilibatilisha uamuzi wa kurudisha kesi kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka na kuagiza kesi iendelee kusikilizwa

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Sala yetu ni kwamba Yehova aendelee kuwa ‘nguvu na ngao’ kwa Valentina, Tatyana, na ndugu na dada wengine wote ambao wanateswa nchini Urusi na Crimea.​—Zaburi 28:7.