Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Dada Margarita Moiseyenko na mume wake, Konstantin; Dada Galina Yatsik; na Dada Yelena Yatsyk

SEPTEMBA 14, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: SEPTEMBA 22, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAMEFUNGWA | Dada Watatu Wanaimarishwa na Sala

HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAMEFUNGWA | Dada Watatu Wanaimarishwa na Sala

Septemba 21, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Zeya katika Eneo la Amur ilimhukumu Dada Margarita Moiseyenko kifungo cha nje cha miaka mitatu, Dada Galina Yatsik kifungo cha nje cha miaka miwili, na Dada Yelena Yatsyk kifungo cha nje cha miaka miwili na nusu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Mambo ambayo dada zetu wamekabili yanatukumbusha kwamba Yehova husikiliza sala zetu naye atatusaidia kusitawisha sifa tunazohitaji ili kukabiliana na jaribu lolote.​—1 Yohana 5:14.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 21, 2019

    Nyumba ya akina Moiseyenkos yafanyiwa upekuzi

  2. Oktoba 13, 2020

    Nyumba ya Yelena na Galina zafanyiwa upekuzi

  3. Novemba 22, 2021

    Kesi ya uhalifu yafunguliwa

  4. Februari 15, 2022

    Anawekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Aprili 24, 2023

    Kesi ya uhalifu yaanza

a Dada Galina Yatsik na Dada Yelena Yatsyk hawana uhusiano wa ukoo.