Hamia kwenye habari

Dada Anna Safronov

JANUARI 28, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Dada Anna Safronova Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Sita

Hukumu Kali na Ndefu Zaidi Kupewa Dada Tangu Marufuku ya 2017

HABARI ZA KARIBUNI | Dada Anna Safronova Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Sita

Aprili 14, 2022, Mahakama ya Eneo la Astrakhan ilikataa rufaa ya Dada Anna Safronova. Ataendelea kukaa gerezani.

Januari 25, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Trusovskiy katika Eneo la Astrakhan ilimhukumu Anna, mwenye umri wa miaka 56, kifungo cha miaka sita gerezani. Alipelekwa kizuizini mara moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 28, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa

  2. Juni 2, 2021

    Wenye mamlaka walifanya upekuzi katika nyumba anayoishi na mama yake mwenye umri wa miaka 81. Anna aliwekwa kizuizini

  3. Juni 3, 2021

    Aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani. Alizuiwa asiondoke nyumbani kwake isipokuwa tu kwenda matembezi kwa saa moja kwa siku, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi

  4. Juni 10, 2021

    Aliongezwa kwenye orodha ya watu wenye msimamo mkali na akaunti zake za benki zikafungwa

  5. Januari 24, 2022

    Katika maelezo yake ya kumalizia mahakamani alisema hivi: “Yesu aliwafundisha wafuasi wake katika Mathayo 5:44 ‘wawapende adui zao na kusali kwa ajili ya wale wanaowatesa.’ Kwa nini? Kwa sababu kuna mifano mingi ya watu waliokuwa wakiwatesa lakini baadaye wakawa waabudu wa Yehova.

    “Ninatumaini kwamba angalau ofisa mmoja wa FSB, mpelelezi, mlinzi, wakili, au yeyote anayenisikia na kuona tabia zangu atabadili mtazamo wake kuelekea Mashahidi wa Yehova . . . Huenda angalau mtu mmoja atataka kusoma Biblia, atafute majibu ya maswali, na kusitawisha tamaa ya kumjua Mungu, au hata kuwa mtumishi wake.”

  6. Januari 25, 2022

    Alishtakiwa na kuhukumiwa miaka sita gerezani

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunatiwa moyo na mifano ya uaminifu ya ndugu na dada zetu nchini Urusi na Crimea tunapoendelea kumtegemea Baba yetu wa mbinguni ili tupate nguvu za kuvumilia.​—2 Wathesalonike 1:4.

a Alihojiwa kabla ya kuhukumiwa.