Hamia kwenye habari

MEI 12, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Dada Svetlana Monis Ameshindwa Kesi ya Rufaa

HABARI ZA KARIBUNI | Dada Svetlana Monis Ameshindwa Kesi ya Rufaa

Machi 9, 2022, Mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi ilibatilisha hukumu ya Dada Svetlana Monis. Kesi yake sasa itapelekwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Birobidzhansky ya Eneo Lililotengewa Wayahudi ili isikilizwe tena.

Mei 12, 2021, Mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi ilikataa rufaa ya Dada Monis. Mahakama ya Urusi iliunga mkono ombi la mwendesha-mashtaka la kubadili hukumu ya awali ya Svetlana, yaani, faini ya rubo 10,000 (dola 135 za Marekani), kuwa kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.