DESEMBA 8, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA FEBRUARI 15, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—FAINI ZAPUNGUZWA | Wana Uhakika Yehova Anawategemeza
Februari 13, 2023, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Chuvash iliwapunguzia Dada Nina Martynova na Dada Zoya Pavlova faini walizotozwa kutoka rubo 350,000 (dola 4,780 za Marekani) hadi rubo 80,000 (dola 1,092 za Marekani). Hukumu ya kifungo cha nje walichopewa Ndugu Andrey Martynov na Ndugu Mikhail Yermakov haikubadilishwa.
Desemba 22, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Alatyrskiy iliyo katika Jamhuri ya Chuvash iliwahukumu Andrey, Nina, Zoya, na Mikhail. Nina and Zoya walitozwa rubo 350,000 (dola 4,780 za Marekani) kila mmoja. Andrey na Mikhail walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Kama ndugu na dada zetu wanaoendelea kuwa imara licha ya mateso, sisi pia tunaweza kuwa na “ujasiri kama simba” tunapokabili majaribu, tukiwa na uhakika kwamba Yehova anatupenda na atatugemeza.—Methali 28:1.
Mfuatano wa Matukio
Juni 23, 2021
Nyumba kadhaa zilifanyiwa msako huko Alatyr
Oktoba 28, 2021
Andrey alianza kuchunguzwa kwa madai kwamba alipanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali. Aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Aprili 25, 2022
Andrey alishtakiwa rasmi. Nina aliongezwa kwenye kesi na akashtakiwa kwa kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Aprili 26, 2022
Zoya alishtakiwa rasmi kwa kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali na akaongezwa kwenye kesi
Aprili 28, 2022
Mikhail alishtakiwa rasmi kwa kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali na akaongezwa kwenye kesi
Agosti 31, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza