Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia, safu ya juu: Ndugu Sergey Agadzhanov; Dada Lyubov Asatryan, Dada Galina Dergacheva, na Dada Inna Kardakova

Safu ya katikati: Dada Irina Khvostova na Dada Galina Pechko; Ndugu Konstantin Petrov, Ndugu Ivan Puyda, na Ndugu Viktor Revyakin

Safu ya chini: Ndugu Mikhail Solntsev na mke wake, Oksana; Ndugu Sergey Yerkin na Ndugu Yevgeniy Zyablov

OKTOBA 17, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: MACHI 7, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU | Kesi ya Mashahidi Kumi na Watatu Yasikilizwa Jijini Magadan

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU | Kesi ya Mashahidi Kumi na Watatu Yasikilizwa Jijini Magadan

Machi 6, 2024, Mahakama ya Jiji la Magadan iliyo katika Eneo la Magadan iliwahukumu ndugu na dada wafuatao: Sergey Agadzhanov, Lyubov Asatryan, Galina Dergacheva, Inna Kardakova, Irina Khvostova, Galina Pechko, Konstantin Petrov, Ivan Puyda, Viktor Revyakin, Mikhail Solntsev, Oksana Solntseva, Sergey Yerkin, na Yevgeniy Zyablov.

Ndugu Sergey Agadzhanov, Lyubov, Galina Dergacheva, Inna, Irina, Galina Pechko, Viktor, Mikhail, na Oksana walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu. Yevgeniy alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano. Konstantin, Ivan, na Sergey Yerkin walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka saba. Ndugu na dada hao hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 30, 2018

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Ivan, Konstantin, Sergey Yerkin, na Yevgeniy kwa shtaka la kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  2. Juni 1, 2018

    Ndugu hao wanne waliwekwa mahabusu

  3. Agosti 3, 2018

    Konstantin aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  4. Oktoba 5, 2018

    Ivan, Sergey Yerkin, na Yevgeniy waliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  5. Machi 20, 2019

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Sergey Agadzhanov, Galina Dergacheva, Inna, Irina, Lyubov, Mikhail, Oksana, na Viktor. Kisha wote hao waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Machi 27, 2019

    Ivan, Konstantin, Sergey Yerkin, na Yevgeniy waliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  7. Aprili 1, 2019

    Wenye mamlaka waliunganisha kesi hizo za uhalifu

  8. Machi 2, 2021

    Galina Pechko aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  9. Machi 5, 2021

    Galina Pechko alishtakiwa kwa kushiriki utendaji wa shirika lenye msimamo mkali na kesi yake iliunganishwa na kesi ya ndugu na dada wengine 12

  10. Aprili 25, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunatiwa moyo sana tunapowaona ndugu na dada zetu wakiendelea kuwa na shangwe licha ya ‘kushutumiwa kwa ajili ya jina la Kristo, huku roho ya Mungu, ikiwa imetulia juu yao.’​—1 Petro 4:14.

a Hatukuweza kupata maelezo kutoka kwa Ndugu Sergey Agadzhanov.