Hamia kwenye habari

Safu ya juu (kushoto hadi kulia): Ndugu Ivan Chaykovskiy na Ndugu Yuriy Chernyshev

Safu ya chini (kushoto hadi kulia): Ndugu Vitaliy Komarov, Ndugu Sergey Shatalov, na Ndugu Vardan Zakaryan

JUNI 7, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: APRILI 3, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YA GEREZANI | Kumtegemea Yehova Kunawasaidia Akina Ndugu Kuvumilia

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YA GEREZANI | Kumtegemea Yehova Kunawasaidia Akina Ndugu Kuvumilia

Machi 31, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Babushkinskiy ya Moscow iliwahukumu Ndugu Ivan Chaykovskiy, Ndugu Yuriy Chernyshev, Ndugu Vitaliy Komarov, na Ndugu Sergey Shatalov vifungo vya miaka sita na miezi mitatu gerezani. Ndugu Vardan Zakaryan alihukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi mitatu gerezani. Walipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 24, 2020

    Maofisa wa polisi nchini Urusi walivamia nyumba 20 hivi za Mashahidi wa Yehova jijini Moscow. Maofisa hao waliwapeleka kizuizini Ivan, Yuriy, Vitaliy, na Sergey na kila mmoja akafungiwa katika chumba tofauti cha gereza. Wanahabari walikuwepo wakati nyumba ya Yuriy ilipokuwa ikipekuliwa na yeye na familia yake kuhojiwa. Baadaye habari walizokusanya zilionyeshwa kwenye vituo vya televisheni vinavyomilikiwa na Serikali

  2. Novemba 26, 2020

    Sergey aliachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani. Vardan, aliyekuwa amelazwa hospitalini kwa sababu ya majeraha aliyopata wakati wa uvamizi huo, alipelekwa mahabusu na kuwekwa kwenye chumba cha gereza akiwa ametengwa na wengine

  3. Novemba 27, 2020

    Mahakama iliwaachilia Ivan, Yuriy, na Vitaliy kutoka kizuizini na kuwaweka chini ya kifungo cha nyumbani

  4. Novemba 30, 2020

    Wenye mamlaka walimwachilia Vardan kutoka mahabusu na wakamweka chini ya kifungo cha nyumbani. Baada ya hayo, Vardan alituma malalamiko kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka kuhusu jinsi maofisa walivyotumia mabavu kwa njia isiyo halali walipokuwa wakifanya upekuzi

  5. Februari 16, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunatiwa moyo tunapoona kwamba Yehova anaendelea kuwakaribia ndugu na dada zetu wapendwa pamoja na familia zao kwa sababu wanajitahidi sana kumkaribia.​—Yakobo 4:8.