Hamia kwenye habari

Ndugu Pavel Brilkov

NOVEMBA 15, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: MACHI 13, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YABADILISHWA | “Nimeazimia Kumtegemea Yehova”

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YABADILISHWA | “Nimeazimia Kumtegemea Yehova”

JMachi 12, 2024, Mahakama ya Mkoa wa Kemerovo ilibadili hukumu ya Ndugu Pavel Brilkov baada ya kukata rufaa. Hukumu yake ya mwanzo ya kazi ngumu gerezani alibadilishwa na kuwa kifungo cha nyumbani cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Januari 15, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Prokopyevsk ilikuwa imemhukumu Ndugu Pavel Brilkov kifungo cha miaka miwili na miezi kumi ya kazi ngumu. a Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Ingawa tunasikitishwa na mateso ambayo ndugu na dada zetu wanakabili, tumeazimia kuonyesha “mtazamo wa kumngojea Mungu wa wokovu” wetu tunapotazamia baraka za wakati ujao kwa uhakika.​—Mika 7:7.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 10, 2021

    Nyumba yao ilifanyiwa upekuzi. Pavel na Vera walihojiwa

  2. Mei 30, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa

  3. Machi 16, 2023

    Waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Mei 25, 2023

    Kesi ya uhalifu inaanzaN

a Mtu anayepewa adhabu ya kufanya kazi ya kulazimishwa hupewa kazi ya kufanya na wenye mamlaka kisha mapato yake yanaweza kukatwa kwa asilimia 5 hadi 20. Ikiwa wenye mamlaka wataamua kwamba mtu huyo hana ushirikiano au anakataa kufanya kazi, basi anaweza kupelekwa gerezani.