Hamia kwenye habari

Dada Yelena Menchiko

DESEMBA 21, 2021| HABARI ZILIONGEZWA: DESEMBA 6, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YABATILISHWA | Dada Yelena Menchikova Ameimarishwa na Mifano ya Uaminifu na Kusali kwa Rafiki Yake Mpendwa, Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YABATILISHWA | Dada Yelena Menchikova Ameimarishwa na Mifano ya Uaminifu na Kusali kwa Rafiki Yake Mpendwa, Yehova

Desemba 5, 2022, Mahakama ya Tano ya Kuchunguza Upya Maamuzi ya Mahakama za Chini ilibatilisha hukumu ya Dada Yelena Menchikova. Kesi yake itarudishwa ili kusikilizwa upya.

Februari 15, 2022, Mahakama Kuu katika Jamhuri ya Karachayevo-Circassian ilikataa ombi la rufaa la Yelena. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 15, 2021

    Mahakama ya Jiji la Cherkessk katika Jamhuri ya Karachayevo-Circassian ilimhukumu Yelena kifungo cha nje cha miaka mitano

  2. Juni 9, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza kusikilizwa

  3. Machi 9, 2021

    Mpelelezi alifungua kesi ya pili ya uhalifu, pindi hii akidai Yelena “alianzisha mpango wa uhalifu” wa kuwahusisha wengine katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  4. Februari 10, 2021

    Mpelelezi alikataa ombi la Yelena la kufuta kesi hiyo baada ya Yelena kunukuu mistari ya Biblia kueleza kwa nini alifanya hivyo. Kulingana na mpelelezi huyo, matumizi yake ya mistari ya Biblia ndiyo iliyothibitisha utendaji wake ni “utendaji wa kihalifu”

  5. Novemba 13, 2020

    Mpelelezi alimfungulia kesi ya uhalifu kwa sababu ya kuimba nyimbo na kusali kwa Yehova

  6. Novemba 12, 2020

    Wenye mamlaka walifanya upekuzi katika nyumba ya Yelena kwa mara ya pili

  7. Desemba 16, 2019

    Maofisa wa FSB katika jiji la Cherkessk walifanya upekuzi katika nyumba za familia kumi za Mashahidi wa Yehova, kutia ndani nyumba ya Yelena

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunasali kwamba Yehova ataendelea kumfariji na kumwimarisha Yelena pamoja na watumishi wake wote washikamanifu wanaokabili majaribu.​—Zaburi 119:49, 50.