Hamia kwenye habari

Ndugu Oleg Postnikov na mke wake, Agnessa

DESEMBA 23, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI— HUKUMU YAFUTWA | Maandalizi ya Yehova Yanaipa Amani Familia ya Postnikov

HABARI ZA KARIBUNI— HUKUMU YAFUTWA | Maandalizi ya Yehova Yanaipa Amani Familia ya Postnikov

Oktoba 11, 2022, Mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi ilipindua uamuzi wa hukumu iliyotolewa dhidi ya Ndugu Oleg Postnikov na Dada Agnessa Postnikova. Kesi yao itasikilizwa upya.

Aprili 25, 2022, Mahakama ya Jiji la Birobidzhan katika Eneo Lililotengewa Wayahudiilimhukumu Oleg kifungo cha nje cha miaka mitano na nusu na Agnessa miaka mitano. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 12, 2021

    FSB ilianzisha kesi ya uhalifu dhidi ya Agnessa. Familia ya Postnikov ilishtakiwa kwamba imeanzisha kikundi cha “wahalifu” na kwamba wanawatangazia wengine malengo yenye “msimamo mkali” ya kikundi hicho. Oleg na Agnessa wamekatazwa kuondoka eneo hilo, akaunti zao za benki zimezuiwa, na majina yao yameongezwa kwenye orodha ya Urusi ya magaidi

  2. Februari 12, 2020

    FSB ilianzisha kesi ya uhalifu dhidi ya Oleg

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Masimulizi hayo yanathibitisha hata zaidi kwamba Yehova amewatayarisha watu wake ili waweze kubaki waaminifu licha ya majaribu mbalimbali. Sote na tuendelee kutegemea ‘upendo mshikamanifu wa Yehova na uaminifu wake.’​—Zaburi 115:1