Hamia kwenye habari

Kutoka kushoto hadi kulia: Ndugu Anton Chermnykh, Ndugu Sergey Korolchuk, na Ndugu Dmitriy Tishchenko

JULAI 14, 2021 | HABARI ZILIONGEZWA: DESEMBA 2, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YATANGAZWA | Kujitayarisha kwa Ajili ya Mateso Kunawasaidia Ndugu Watatu Kudumisha Ushikamanifu

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YATANGAZWA | Kujitayarisha kwa Ajili ya Mateso Kunawasaidia Ndugu Watatu Kudumisha Ushikamanifu

Novemba 30, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Ussuriyskiy katika Eneo la Primorye imewahukumu Ndugu Anton Chermnykh, Ndugu Sergey Korolchuk, na Ndugu Dmitriy Tishchenko vifungo vya nje vya miaka sita. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Septemba 23, 2020

    Kesi dhidi ya Anton, Sergey, na Dmitriy ilianza kusikilizwa mahakamani

  2. Julai 7, 2020

    Anton, Sergey, na Dmitriy walishtakiwa rasmi kwa kuwa viongozi wa shirika la kidini lililopigwa marufuku na lenye “msimamo mkali”

  3. Juni 18, 2019

    Sergey aliwekwa mahabusu kwa siku mbili

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Kesi yao inapoendelea kusikilizwa, tunajua kwamba Yehova atabariki uaminifu wa Anton, Sergey, na Dmitriy.​—Methali 28:20.