Hamia kwenye habari

Kuanzia kushoto hadi kulia: Ndugu Marat Abdulgalimov, Ndugu Arsen Abdullaev, Ndugu Anton Dergalev, na Dada Mariya Karpova

AGOSTI 20, 2021 | HABARI ZILIZOONGEZWA: NOVEMBA 28, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YATANGAZWA | Ndugu Watatu na Dada Mmoja Huko Dagestan Wapokea Utegemezo wa Yehova Wakiwa Kizuizini

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YATANGAZWA | Ndugu Watatu na Dada Mmoja Huko Dagestan Wapokea Utegemezo wa Yehova Wakiwa Kizuizini

Novemba 24, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Kirovskiy iliyo Makhachkala imewahukumu Ndugu Marat Abdulgalimov, Ndugu Arsen Abdullaev, Ndugu Anton Dergalev, na Dada Mariya Karpova. Kila mmoja amepewa kifungo cha nje cha miaka sita au miaka sita na nusu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 27, 2020

    Baada ya siku 362, Marat, Arsen, Anton, na Mariya walihamishwa kutoka mahabusu kwenda kifungo cha nyumbani

  2. Juni 4, 2019

    Mahakama ya Wilaya ya Sovetskiy huko Makhachkala iliwaweka wote mahabusu

  3. Juni 1, 2019

    Maofisa wa FSB, yaani, polisi wa siri wa Urusi, walivamia nyumba 13 za Mashahidi wa Yehova katika eneo lote la Dagestan

  4. Mei 27, 2019

    Ofisi ya FSB katika eneo la Dagestan ilifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Marat, Arsen, Anton, na Mariya

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kamili kwamba sikuzote Yehova Mungu atakuwa kile kinachohitajika ili kuwalinda na kuwategemeza watu wake kama jina lake linavyomaanisha.​—Kutoka 3:14.