Hamia kwenye habari

Kushoto kwenda kulia: Dada Lyubov Galitsyna, Ndugu Garegin Khachaturyan na Ndugu Gevorg Yeritsyan

APRILI 8, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: JULAI 1, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU ZA GEREZANI | Wanauona Mkono wa Yehova Wakiwa Mahabusu

HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU ZA GEREZANI | Wanauona Mkono wa Yehova Wakiwa Mahabusu

Juni 26, 2024, Mahakama ya Jiji la Novocherkassk iliyo katika Eneo la Rostov iliwahukumu Dada Lyubov Galitsyna, Ndugu Garegin Khachaturyan, na Ndugu Gevorg Yeritsyan. Dada Lyubov alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu gerezani, lakini kwa kuwa amekuwa katika kifungo cha nje, kifungo chake kimekamilika. Ndugu Garegin alihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi sita na Ndugu Gevorg akahukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi miwili gerezani. Ndugu wote wawili wataendelea kukaa kifungoni.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba ingawa wapinzani wetu wameazimia kutudhuru, Yehova ataendelea kuwabariki watumishi wake washikamanifu na kufanya “hali hiyo ibadilike na kuwa njema.”​—Mwanzo 50:20

Mfuatano wa Matukio

  1. Agosti 11, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Lyubov, Garegin, na Gevorg. Nyumba zao zilifanyiwa msako. Garegin na Gevorg waliwekwa kizuizini

  2. Agosti 12, 2022

    Garegin na Gevorg walihamishiwa mahabusu

  3. Agosti 16, 2022

    Lyubov aliwekwa kizuizini

  4. Agosti 17, 2022

    Lyubov alihamishiwa mahabusu

  5. Septemba 20, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

  6. Desemba 25, 2023

    Lyubov alitolewa mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

a b Makala hii ilipokuwa ikitayarishwa, Ndugu Khachaturyan na Ndugu Yeritsyan walikuwa mahabusu, hivyo hatukuweza kupata maelezo kutoka kwao.