Hamia kwenye habari

Ndugu Konstantin Sannikov

APRILI 8, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: FEBRUARI 16, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—KIFUNGO CHA GEREZANI | Baba Anashughulikia Mahitaji ya Kiroho ya Familia Yake Akiwa Kifungoni

HABARI ZA KARIBUNI—KIFUNGO CHA GEREZANI | Baba Anashughulikia Mahitaji ya Kiroho ya Familia Yake Akiwa Kifungoni

Februari 15, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Sovetskiy iliyoko Kazan ilimhukumu Ndugu Konstantin Sannikov kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Konstantin amekuwa mahabusu tangu Agosti 2020 na ataendelea kubaki huko.

Mfuatano wa Matukio

  1. Agosti 25, 2020

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa baada ya wapelelezi kuweka vifaa vya kusikiliza kisiri nyumbani kwa Konstantin. Wenye mamlaka walisema kwamba kuruhusu mazungumzo ya Biblia kufanyiwa nyumbani kwake ni kupanga utendaji ulio na msimamo mkali

  2. Agosti 27, 2020

    Alikamatwa na kupelekwa mahabusu mara moja

  3. Mei 26, 2021

    Mahakama ilimzuia mke wake asimtembelee na imeendelea kukataa maombi yake

  4. Agosti 20, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza kusikilizwa

Maelezo Mafupi Kumhusu

Konstantin anapoendelea kuitunza familia yake kiroho akiwa kizuizini, tuna uhakika kwamba Yehova hatakosa kuwatunza “watu wake mwenyewe.”​—1 Timotheo 5:8.

a Kwa kuwa kwa sasa Ndugu Sannikov yuko mahabusu, hatukuweza kupata maelezo kutoka kwake.