Hamia kwenye habari

Dada Lyudmila Salikov

JANUARI 31, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: MACHI 27, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—KIFUNGO CHAPUNGUZWA | Dada Lyudmila Salikova Anapata Nguvu na Faraja Katika Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—KIFUNGO CHAPUNGUZWA | Dada Lyudmila Salikova Anapata Nguvu na Faraja Katika Yehova

Machi 23, 2023, Mahakama ya Eneo la Chelyabinsk ilitangaza uamuzi wake baada ya Dada Lyudmila Salikova kukata rufaa kwa mara ya pili. Mahakama hiyo ilipunguza urefu wa kifungo chake cha nje kutoka miaka sita hadi miaka miwili na nusu. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Machi 17, 2022, Mahakama ya Eneo la Chelyabinsk ilikataa ombi la rufaa la Lyudmila.

Januari 20, 2022, Mahakama ya Jiji la Snezhinsk katika Eneo la Chelyabinsk ilimhukumu Lyudmila kifungo cha nje cha miaka sita.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 2020

    Maofisa wa usalama katika jiji la Snezhinsk walifanya upekuzi katika nyumba za familia nne za Mashahidi wa Yehova, kutia ndani nyumba ya Lyudmila. Pia, maofisa walifanya upekuzi katika eneo lake la kazi. Kwa sababu hiyo, alilazimishwa kujiuzulu kazini

  2. Agosti 26, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Lyudmila kwa sababu ya kupanga shughuli za shirika la kidini lililopigwa marufuku na kuingiza nchini machapisho yaliyopigwa marufuku

  3. Desemba 8, 2021

    Kesi yake ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Ndugu na dada zetu nchini Urusi wanaendelea kupata nguvu na faraja kutoka kwa Yehova. Mungu wetu mwenye upendo anatuhakikishia kwamba atawatendea “haki mayatima na wale wanaopondwa, ili mwanadamu anayeweza kufa ambaye ni mavumbi asiwaogopeshe tena.”​—Zaburi 10:18.