Hamia kwenye habari

Kutoka kushoto hadi kulia: Ndugu Yegor Baranov na Ndugu Yen Sen Li

AGOSTI 13, 2021| HABARI ZILIONGEZWA: MACHI 6, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNIKIFUNGO CHAPUNGUZWA | Ndugu Baranov na Ndugu Li Wanaendelea Kuwa Watulivu na Kuwa na Uhakika Katika Yehova

HABARI ZA KARIBUNIKIFUNGO CHAPUNGUZWA | Ndugu Baranov na Ndugu Li Wanaendelea Kuwa Watulivu na Kuwa na Uhakika Katika Yehova

Machi 1, 2023, Mahakama iliyo katika Eneo la Khabarovsk ilipunguza urefu wa kifungo cha nje cha Ndugu Yegor Baranov hadi miaka minne na nusu baada ya kesi ya rufaa kusikilizwa. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Juni 6, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Vyazemskiy iliyo katika Eneo la Khabarovsk ilimhukumu Yegor kifungo cha nje cha miaka mitano. Kwa kusikitisha, Ndugu Yen Sen Li alikufa kabla ya hukumu kutolewa.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 2, 2021

    Kesi dhidi ya Yegor na Yen Sen ilianza kusikilizwa mahakamani

  2. Novemba 20, 2020

    Yegor aliachiliwa kutoka mahabusu baada ya kukaa humo siku 177

  3. Agosti 26, 2020

    Mahakama ya Wilaya ya Kati iliyoko Khabarovsk ilitwaa gari la Yen Sen

  4. Mei 29, 2020

    Yegor alipelekwa mahabusu

  5. Mei 26, 2020

    Kesi ya uhalifu inafunguliwa dhidi ya Yegor na Yen Sen katika Eneo la Khabarovsk

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunawapongeza ndugu zetu kwa kuendelea kumtegemea Yehova na tuna uhakika kwamba atawaimarisha waweze kuvumilia.​—2 Wathesalonike 3:3.