Hamia kwenye habari

Ndugu Anatoliy Gorbunov na mke wake, Galina

AGOSTI 5, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Kudumu Katika Sala Kunamsaidia Ndugu Anatoliy Gorbunov Kudumisha Shangwe

HABARI ZA KARIBUNI | Kudumu Katika Sala Kunamsaidia Ndugu Anatoliy Gorbunov Kudumisha Shangwe

Juni 21, 2022, Mahakama ya Eneo la Krasnoyarsk ilikataa rufaa ya Ndugu Anatoliy Gorbunov na ikaunga mkono hukumu aliyopewa. Hivi karibuni atahamishiwa gereza lingine.

Februari 2, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Oktyabr’skiy iliyo katika Jiji la Krasnoyarsk ilimhukumu Ndugu Anatoliy Gorbunov kifungo cha miaka sita gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 9, 2021

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Anatoliy inaanza

  2. Septemba 15, 2020

    Nyumba ya Anatoliy inafanyiwa upekuzi kwa mara ya pili. Wenye mamlaka walichukua funguo za nyumba yao

  3. Machi 25, 2020

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Anatoliy inaanza. Alishtakiwa kwa kupanga mikutano ya kidini ya shirika lililopigwa marufuku

  4. Novemba 7, 2018

    Nyumba ya Anatoliy inafanyiwa upekuzi mapema asubuhi. Wenye mamlaka wanachukua kompyuta ndogo, tablet, flash drive, hard drive, na simu mbili. Anatoliy alifikishwa kwenye Kamati ya Uchunguzi ya Shirikisho la Urusi ili ahojiwe kisha akaachiliwa baada ya saa moja

Maelezo Mafupi Kumhusu

Anatoliy na familia yake wanapoendelea kumtegemea Yehova kwa kusali kwake, tuna uhakika kwamba atawategemeza na kuwasaidia kudumisha shangwe yao.​—Zaburi 25:1, 2.