Hamia kwenye habari

Ndugu Andrey Vlasov

FEBRUARI 2, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Kuendelea Kuwa Mtendaji Kunamsaidia Ndugu Andrey Vlasov Kudumisha Mtazamo Mzuri

HABARI ZA KARIBUNI | Kuendelea Kuwa Mtendaji Kunamsaidia Ndugu Andrey Vlasov Kudumisha Mtazamo Mzuri

Julai 26, 2022, Mahakama ya Eneo la Kemerovo ilikataa rufaa ya Ndugu Andrey Vlasov. Ataendelea kukaa gerezani.

Mei 23, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Kati katika Jiji la Prokopyevsk ilimhukumu Andrey kifungo cha miaka saba gerezani. Hukumu hiyo itaanza kutumika mara moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 2, 2020

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa dhidi ya Andrey kwa sababu alishukiwa kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  2. Julai 12, 2020

    Maofisa wa FSB walifanya upekuzi nyumbani na kazini kwa Andrey. Walichukua vifaa vya kielektroni na Biblia. Alipelekwa kizuizini huku wapelelezi wakimhoji mke wake, Nataliya

  3. Julai 14, 2020

    Aliachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  4. Juni 9, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Ni pendeleo kubwa kuwa wafanyakazi wenzi wa Andrey na ndugu na dada wengine nchini Urusi na Crimea wanapoendelea kudumisha shangwe yao na kusimama imara katika imani.​—2 Wakorintho 1:24.