Hamia kwenye habari

Kuanzia juu kushoto: Dada Maya Karpushkina; Ndugu Nikolay Polevodov; Ndugu Vitaliy Zhuk na mke wake, Tatyana; Ndugu Stanislav Kim; Dada Svetlana Sedova

MACHI 23, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: OKTOBA 11, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—MAHAKAMA YA RUFAA YATENGUA HUKUMU YA KUFUNGWA GEREZANI | Yehova Anaendelea Kuwategemeza Ndugu na Dada Sita Waaminifu

HABARI ZA KARIBUNI—MAHAKAMA YA RUFAA YATENGUA HUKUMU YA KUFUNGWA GEREZANI | Yehova Anaendelea Kuwategemeza Ndugu na Dada Sita Waaminifu

Oktoba 10, 2024, Mahakama ya Eneo la Khabarovsk ilitangaza uamuzi wake katika kesi ya rufaa iliyowasilishwa na Dada Maya Karpushkina, Ndugu Stanislav Kim, Ndugu Nikolay Polevodov, Dada Svetlana Sedova, Ndugu Vitaliy Zhuk, na Tatyana, mke wake. Vifungo vya nje ambavyo Maya, Svetlana, na Tatyana walikuwa wamehukumiwa vilipunguzwa kwa mwaka mmoja. Kifungo cha gerezani ambacho Stanislav alikuwa amehukumiwa kilitenguliwa na kuwa kifungo cha nje cha miaka saba na miezi miwili, nacho cha Vitaliy kikawa kifungo cha nje cha miaka saba na miezi minne, na cha Nikolay kikawa kifungo cha nje cha miaka saba na miezi sita. Ndugu hao waliachiliwa kutoka gerezani baadaye siku hiyo.

Juni 20, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy iliyo katika Eneo la Khabarovsk iliwahukumu Dada Maya Karpushkina, Ndugu Stanislav Kim, Ndugu Nikolay Polevodov, Dada Svetlana Sedova, Ndugu Vitaliy Zhuk, na mke wake, Tatyana. Maya alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka minne. Svetlana na Tatyana walipokea hukumu ya kifungo cha nje cha miaka mitano kila mmoja. Dada hao hawahitaji kwenda gerezani wakati huu. Stanislav alihukumiwa kifungo cha miaka minane na miezi miwili gerezani, Vitaliy alihukumiwa kifungo cha miaka minane na miezi minne, na Nikolay alihukumiwa kifungo cha miaka minane na miezi sita. Hivi ni vifungo virefu zaidi tangu marufuku iliyotangazwa mwaka wa 2017. Akina ndugu walipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 10, 2018

    Wenye mamlaka walivuruga tafrija ya watu 55 hivi katika mkahawa. Watu wote waliohudhuria kutia ndani watoto walihojiwa, alama za vidole zikachukuliwa, na wakapigwa picha

  2. Novemba 12, 2018

    Stanislav, Nikolay, na Vitaliy walipelekwa mahabusu. Maya, Svetlana, na Tatyana waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Januari 14, 2019

    Nikolay na Vitaliy walitolewa mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  4. Januari 29, 2019

    Stanislav alitolewa mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  5. Julai 18, 2019

    Kesi hiyo iliwasilishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy iliyo katika Eneo la Khabarovsk

  6. Agosti 2, 2019

    Nikolay aliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani

  7. Septemba 9, 2019

    Kesi tofauti iliyowahusisha Stanislav na Nikolay iliwasilishwa kwenye Mahakama ya Zheleznodorozhniy iliyo katika Eneo la Khabarovsk

  8. Novemba 5, 2019

    Nikolay aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  9. Januari 18, 2020

    Stanislav na Vitaliy waliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani

  10. Februari 4, 2020

    Stanislav na Nikolay walihukumiwa katika ile kesi tofauti kuwa wenye hatia. Mahama ya Wilaya ya Zheleznodorozhniy iliyo Khabarovsk iliwapa kila mmoja wao kifungo cha nje cha miaka miwili ili kuwachunguza tabia

  11. Agosti 3, 2020

    Kesi iliyokuwa katika Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy ilirudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka. Basi mwendesha-mashtaka akaamua kukata rufaa

  12. Septemba 29, 2020

    Mahakama ya Eneo la Khabarovsk ilikubali rufaa ya mwendesha-mashtaka. Stanislav na Nikolay waliruhusiwa kujieleza mbele ya hakimu. Walisema kwamba kama vile tu mataifa mengine Shirikisho la Urusi limeahidi kutokiuka haki za raia wake na uhuru wao wa kuabudu

  13. Oktoba 12, 2020

    Mahakama ya Eneo la Khabarovsk iliunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy na kurudisha kesi kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka

  14. Desemba 15, 2021

    Kesi iliwasilishwa tena kwenye Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza ndugu na dada hawa wapendwa na wengine wengi ambao wanafanyiza ‘wingu kubwa la mashahidi.’​—Waebrania 12:1.