Hamia kwenye habari

Ndugu Pyotr Krupnov na mke wake, May

JANUARI 4, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Maandalizi na Tumaini Yamewasaidia Ndugu Pyotr Krupnov na Mke Wake, Maya

HABARI ZA KARIBUNI | Maandalizi na Tumaini Yamewasaidia Ndugu Pyotr Krupnov na Mke Wake, Maya

Machi 9, 2022, Mahakama ya Eneo la Penza ilikataa rufaa ya Ndugu Pyotr Krupnov na mke wake, Maya. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Wakati

  1. Desemba 30, 2021

    Mahakama ya Wilaya ya Nikolskiy katika Eneo la Penza iliwahukumu Pyotr na mke wake, Maya, kifungo cha nje cha miaka mitatu.

  2. Oktoba 25, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza kusikilizwa

  3. Oktoba 12, 2021

    Pyotr na Maya waliongezwa kwenye orodha ya magaidi na watu wenye msimamo mkali kwa sababu ya kuzungumzia habari za kidini pamoja na rafiki zao

  4. Septemba 15, 2021

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Maya inaanzishwa. Baadaye Pyotr aliongezwa kwenye orodha ya washtakiwa

  5. Oktoba 11, 2020

    Maofisa wa usalama wanafanya upekuzi katika nyumba za familia nne za Mashahidi wa Yehova jijini Nikolsk, kutia ndani nyumba ya Krupnov

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunathamini sana mfano wa Pyotr na Maya ambao wanaendelea kuwa na tumaini imara kama nanga na kumtegemea Yehova.​—Waebrania 6:19.