Hamia kwenye habari

Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Moskovskiy iliyoko Nizhny Novgorod; Picha ndogo: Ndugu Maksim Zavrazhnov

APRILI 20, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Maksim Zavrazhnov Anadumisha Mtazamo Mzuri

HABARI ZA KARIBUNI | Maksim Zavrazhnov Anadumisha Mtazamo Mzuri

Mei 30, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Moskovskiy ya Jiji la Nizhny Novgorod ilimhukumu Ndugu Maksim Zavrazhnov kifungo cha nje cha miaka sita. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Juni 4, 2019

    Upelelezi wa uhalifu unaanzishwa

  2. Julai 17, 2019

    Anashtakiwa rasmi kwa kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali. Anakamatwa, anahojiwa, na kuzuiliwa usiku mzima

  3. Julai 18, 2019

    Anawekewa vizuizi vya kutumia simu, Intaneti, na pia kwamba anapaswa kuwa nyumbani kati ya saa 3:00 usiku na saa 3:00 asubuhi

  4. Februari 3, 2020

    Vizuizi vinaondolewa

  5. Februari 26, 2020

    Anawekewa kizuizi cha kusafiri nje ya eneo la kwao

  6. Desemba 6, 2021

    Kesi ya uhalifu inaanza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kadiri ndugu zetu wapendwa wanavyoendelea kuteswa nchini Urusi na Crimea, uhakika wetu katika Yehova unaimarishwa. Tunajua kwamba hatawaacha kamwe washikamanifu wake.​—Waebrania 13:5.