Hamia kwenye habari

Kushoto: Ndugu Yuriy Baranov na mke wake, Nadezhda. Kulia: Ndugu Nikolay Stepanov na mke wake, Alla

JUNI 8, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNINDUGU AACHILIWA | Alisaidiwa na Waabudu Wenzake

HABARI ZA KARIBUNINDUGU AACHILIWA | Alisaidiwa na Waabudu Wenzake

Novemba 10, 2022, Mahakama ya Eneo la Vologda ilitangaza uamuzi wake katika kesi ya rufaa ya Ndugu Yuriy Baranov na Ndugu Nikolay Stepanov. Hukumu ya ndugu Yuriy haijabadilika. Hukumu ya mapema ya Nikolay ya kifungo cha miaka minne gerezani ilipunguzwa na kuwa kifungo cha nje cha miaka minne. Aliachiliwa mara moja kutoka gerezani.

Septemba 5, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Vologodskiy iliyo katika Eneo la Vologda ilimhukumu Yuriy na Nikolay. Yuriy alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka minne. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu. Nikolay alihukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani. Hukumu hiyo ilitekelezwa mara moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 19, 2019

    Maofisa wa usalama walivamia nyumba sita za familia za Mashahidi wa Yehova katika eneo la Vologda. Ndugu Yuriy na Ndugu Nikolay walikamatwa na kuwekwa kizuizini.

  2. Desemba 20, 2019

    Ndugu Yuriy aliachiliwa na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  3. Desemba 23, 2019

    Ndugu Nikolay alipelekwa mahabusu

  4. Machi 16, 2020

    Ndugu Yuriy aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani, lakini hakuruhusiwa kuwasiliana na wengine ambao walishtakiwa pamoja naye katika kesi ya uhalifu, na hakuruhusiwa kutumia simu au Intaneti

  5. Mei 19, 2020

    Ndugu Yuriy aliondolewa vizuizi

  6. Agosti 13, 2020

    Ndugu Nikolay aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani

  7. Septemba 25, 2020

    Ndugu Nikolay aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani

  8. Machi 7, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Kuwaona akina ndugu wakiendelea kudumisha imani yao ingawa wanateswa, kunaimarisha imani sana.​—1 Wathesalonike 3:7.