MEI 3, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 13, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AFUNGWA | “Macho ya Yehova Yananitazama”
Desemba 7, 2023,Mahakama ya Wilaya ya Kirovskiy iliyo katika jiji la Kazan imemhukumu Ndugu Aleksey Gerasimov kifungo cha miaka sita gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunajua kwamba Yehova hatawaacha watumishi wake washikamanfu. Yeye ni mwaminifu naye hutusaidia kuvumilia jaribu lolote.—1 Wakorintho 10:13.
Mfuatano wa Matukio
Februari 10, 2022
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa
Machi 18, 2022
Nyumba yake ilifanyiwa msako naye alihojiwa
Septemba 23, 2022
Aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Februari 22, 2023
Kifungo cha uhalifu kilianza