Hamia kwenye habari

Ndugu Dmitriy Barmakin na mke wake, Yelena

NOVEMBA 1, 2021 | HABARI ZILIONGEZWA: APRILI 27, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AFUNGWA | Ndugu Dmitriy Barmakin Adumisha Shangwe Yake Licha ya Kuwa Mahabusu kwa Muda Mrefu

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AFUNGWA | Ndugu Dmitriy Barmakin Adumisha Shangwe Yake Licha ya Kuwa Mahabusu kwa Muda Mrefu

Aprili 27, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Pervorechenskiy iliyo Vladivostok katika Eneo la Primorye ilimhukumu Ndugu Dmitriy Barmakin kifungo cha miaka nane gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.

Aprili 8, 2022, Mahakama ya Eneo la Primorye ilibadili uamuzi uliokuwa umetolewa wa kumwondolea hatia Dmitriy. Kesi yake itaanza kusikilizwa upya.

Mfuatano wa Matukio

 
  1. Novemba 22, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Pervorechenskiy iliyo Vladivostok katika Eneo la Primorye, ilitangaza kwamba Dmitriy hana hatia na ikamwondolea mashtaka yote ya uhalifu. Hii ndio mara ya kwanza mahakama ya Urusi imetangaza kwamba Shahidi wa Yehova hana hatia chini ya kifungu cha 282.2(1) cha Sheria ya Uhalifu ya Urusi (kuhusu kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali). Mahakama itamwondolea vizuizi vyote alivyokuwa amewekewa. Hukumu hiyo itatekelezwa Desemba 3, 2021, ikiwa ofisi ya mwendesha-mashtaka haitakata rufaa

  2. Aprili 20, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza kusikilizwa tena

  3. Desemba 18, 2020

    Kesi ya uhalifu ilirudishwa kwa mwendesha-mashtaka kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi wa kutosha. Vizuizi kuhusu utendaji wake bado viliendelea kuwepo

  4. Oktoba 18, 2019

    Baada ya siku 447, Dmitriy aliachiliwa lakini akawekewa vizuizi vikali vya utendaji wake. Mahakama iliongeza mara kumi muda wa Dmitriy kuzuiliwa mahabusu

  5. Julai 28, 2018

    Saa 1:00 asubuhi Julai 28, 2018, kikundi cha wanaume waliokuwa na silaha na waliofunika nyuso zao waliingia kwa nguvu katika nyumba ambayo Dmitriy na Yelena walikuwa wakimtunzia nyanya ya Yelena mwenye umri wa miaka 90. Dmitriy na Yelena walirudishwa katika jiji la nyumbani kwao lililoko umbali wa kilomita 177 huko Vladivostok. Dmitriy alikamatwa na kuwekwa mahabusu mara moja

  6. Julai 27, 2018

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Ndugu Dmitriy Barmakin

  7. Oktoba 2017

    Mwanamke mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) alijifanya kuwa anapendezwa kujifunza Biblia. Alirekodi kisiri video ya mazungumzo yake akiwa na ndugu na dada mbalimbali

Maelezo Mafupi Kumhusu

Ingawa Dmitriy na Yelena wametenganishwa tena na vyuma vya gereza, wenzi hao wa ndoa wanatuwekea mfano mzuri wa kufanya ‘shangwe ya Yehova iwe ngome yao.’​—Nehemia 8:10.