Hamia kwenye habari

Ndugu Boris Yagovitov na mke wake, Nataliya

SEPTEMBA 30, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Anapambana na Hisia za Kuvunjika Moyo kwa Kuwa na Mtazamo Mzuri

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Anapambana na Hisia za Kuvunjika Moyo kwa Kuwa na Mtazamo Mzuri

Oktoba 10, 2022, Solnechniy District Court of the Khabarovsk Territory Mahakama ya Wilaya ya Solnechniy iliyo katika Eneo la Khabarovsk ilimhukumu Ndugu Boris Yagovitov kifungo cha nje cha miaka mitano. Alikuwa mahabusu kwa miezi tisa. Hukumu ilipotolewa aliachiliwa mara moja na hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 14, 2020

    Wapelelezi walitumia sauti zilizorekodiwa za mazungumzo kati ya Boris na ofisa wa polisi aliyejifanya anapendezwa na ujumbe wa Biblia

  2. Mei 14, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Boris. Alishtakiwa kwa kushiriki mikutano ya shirika lenye msimamo mkali na kujaribu kuwashawishi wengine kujiunga na shirika hilo

  3. Juni 5, 2021

    Boris na Nataliya walihojiwa na nyumba yao ilifanyiwa msako. Baada ya hapo Boris alipelekwa mahabusu

  4. Juni 7, 2021

    Aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani

  5. Desemba 29, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza. Kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa mwendesha-mashtaka alidai kwamba Boris hakutii masharti ya kifungo cha nyumbani na hivyo alitaka Boris awekwe mahabusu. Wenye mamlaka walimpeleka mahabusu

  6. Februari 24, 2022

    Kesi ilirudishwa kwa mwendesha-mashtaka kwa sababu wapelelezi hawakufuata utaratibu waliopaswa kufuata. Hata hivyo, Boris hakuachiliwa kutoka mahabusu

  7. Juni 9, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza tena

Maelezo Mafupi Kumhusu

Boris na Nataliya wametuwekea mfano mzuri wa kukazia fikira mambo yaliyo ya uadilifu na yanayostahili sifa. Tuna uhakika kwamba “Mungu wa amani” ataendelea kuwa pamoja nao.​—Wafilipi 4:8, 9.

a Makala hii ilipokuwa ikitayarishwa Ndugu Yagovitov alikuwa mahabusu. Hatukuweza kupata maelezo kutoka kwake.