APRILI 4, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: APRILI 9, 2024
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | ‘Jambo Muhimu Ni Kudumisha Urafiki Wangu na Yehova’
Aprili 8, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Avtozavodskiy katika mji wa Tolyatti iliyo katika Eneo la Samara ilimhukumu Ndugu Aleksandr Dolganov kifungo cha miaka mitatu gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Kama Aleksandr, sisi pia tunaona ni muhimu kutumia vizuri wakati wetu katika ‘siku hizi zenye uovu.’—Waefeso 5:15, 16.
Mfuatano wa Matukio
Mei 16, 2023
Nyumba ilifanyiwa msako. Aleksandr alipelekwa kuzuizini
Mei 17, 2023
Aliachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani. Hakuruhusiwa kutumia simu au intaneti
Agosti 10, 2023
Aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Novemba 13, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza