Hamia kwenye habari

Ndugu Anatoliy Senin

SEPTEMBA 26, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: JANUARI 16, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Kuwa Imara Kiroho Kunasaidia Kushinda Woga

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Kuwa Imara Kiroho Kunasaidia Kushinda Woga

Januari 12, 2023, Mahakama ya Jiji la Kyzylskiy katika Jamhuri ya Tuva ilimhukumu Ndugu Anatoliy Senin kifungo cha nje cha miaka sita. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Januari 28, 2021

    Nyumba yake ilivamiwa na baada ya hapo akakamatwa na kupelekwa kizuizini

  2. Januari 30, 2021

    Aliachiliwa na akawekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  3. Machi 27, 2021

    Aliondolewa kifungo cha nyumbani na akawekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Januari 17, 2022

    Alishtakiwa kwamba anapanga utendaji wa Mashahidi wa Yehova

  5. Aprili 6, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunaweza kupata faraja kutokana na maneno ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Mioyo yenu isitaabike wala kuogopa.”​—Yohana 14:27.