MACHI 22, 2023 | HABARI ZILIONGEZWA: APRILI 28, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | “Nimeazimia Kufanya Kile Yehova Anachotaka”
Aprili 28, 2023, Mahakama ya Jiji la Asha iliyo katika Eneo la Chelyabinsk ilimhukumu Ndugu Vadim Fedorov kifungo cha nje cha miaka sita. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Kama Vadim, sisi pia tuna uhakika kwamba Yehova atawabariki na kuwaimarisha wale wanaoendelea kumtumaini na “[kufuata] njia yake.”—Zaburi 37:34.
Mfuatano wa Matukio
Juni 11, 2021
Maofisa wa polisi walivamia nyumba ya Vadim na ya Andrey, mwana wake
Aprili 29, 2022
Vadim alishtakiwa kuwa mhalifu
Desemba 1, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza