Hamia kwenye habari

Ndugu Dmitriy Dolzhikov na mke wake, Marina

MEI 2, 2023 | HABARI ZILIONGEZWA: JULAI 3, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Nimechochewa na Mifano ya Watu Wenye Imani

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Nimechochewa na Mifano ya Watu Wenye Imani

Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyo katika Jiji la Novosibirsk ilimhukumu Ndugu Dmitriy Dolzhikov na kumwamuru kwamba atafanya kazi ngumu kwa miaka mitatu. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu. Hukumu yake inatia ndani asilimia 10 ya mshahara atakaopokea utachukuliwa na serikali katika miaka hiyo mitatu. Pia, haruhusiwi kutoka nje ya mipaka ya jiji.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kumwimarisha Dmitriy na sisi sote kwa kuwa anaiona imani yetu na uvumilivu wetu.​—Ufunuo 2:19.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 13, 2022

    Kesi ya uhalifu yaanzishwa

  2. Septemba 8, 2022

    Makao yake yapigwa msako. Afungwa mahabusu

  3. Septemba 9, 2022

    Alihojiwa na kusafirishwa kwa ndege Chelyabinsk hadi kwenye kituo cha gereza cha Novosibirsk, umbali wa kilomita zaidi ya 1,500 kilomita

  4. Novemba 11, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

  5. Novemba 24, 2022

    Alifunguliwa kutoka mahabusu na kuwekwa kifungo cha nyumbani