Hamia kwenye habari

Ndugu Vadim Gizatulin

NOVEMBA 25, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: DESEMBA 8, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | “Tunajua Kwamba Hatuko Peke Yetu”

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | “Tunajua Kwamba Hatuko Peke Yetu”

Desemba 27, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Metallurgicheskiy katika Jiji la Chelyabinsk ilimhukumu Ndugu Vadim Gizatulin kifungo cha nje cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Sisi pia tunaweza kuwa na uhakika kwamba tunapokabili majaribu, hatuko peke yetu kamwe. Yehova hatawahi kuwaacha watumishi wake waaminifu.​—Zaburi 9:9, 10.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 26, 2019

    Nyumba ya Vadim ilifanyiwa upekuzi wakati wa uchunguzi dhidi ya Ndugu Vladimir Suvorov

  2. Agosti 31, 2021

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Vadim. Alishtakiwa kushiriki katika utendaji wa shirika la kidini lililopigwa marufuku

  3. Oktoba 22, 2021

    Nyumba yao ilifanyiwa upekuzi kwa mara ya pili. Vadim na mke wake walikamatwa wakahojiwe

  4. Julai 14, 2022

    Waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Agosti 18, 2022

    Kesi ya uhalifu inaanza