AGOSTI 10, 2022
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Viktor Shayapov Anavumilia kwa Shangwe kwa Sababu ya Kuwa Mwenye Shukrani
Novemba 7, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Nikolskiy iliyo katika Eneo la Penza ilimhukumu Ndugu Viktor Shayapov kifungo cha nje cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Mfuatano wa Matukio
Agosti 19, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa. Ameshtakiwa kwa kosa la kushiriki utendaji wenye msimamo mkali
Februari 5, 2022
Alisimamishwa na maofisa wa polisi. Siku hiyohiyo nyumba yake ikafanyiwa msako. Aliwekwa kizuizini na kupelekwa umbali wa kilomita 740 katika eneo la Penza
Februari 6, 2022
Aliwekwa mahabusu
Februari 8, 2022
Aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani
Machi 28, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunamshukuru sana Yehova kwa sababu tunajua amani tunayopata kutokana na upendo wake mshikamanifu italinda mioyo na akili zetu hata katika majaribu.—Wafilipi 4:7.