Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Kuznetsov

MAY 5, 2022 | TAREHE YA KARIBUNI DESEMBA 26, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Yehova Amemwimarisha Sergey Kuznetsov

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | Yehova Amemwimarisha Sergey Kuznetsov

Desemba 22, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Vyazemskiy iliyo katika Eneo la Khabarovsk ilimhukumu Ndugu Sergey Kuznetsov kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi mitano. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu

Mfuatano wa Matukio

  1. Septemba 3, 2020

    Maofisa wa FSB walipekua nyumba ya Sergey. Walichukua Biblia, vifaa vya kielektroni, na machapisho

  2. Aprili 2, 2021

    Aliwekwa kwenye orodha ya magaidi. Akaunti zake za Benki zilizuiliwa

  3. Novemba 9, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwaimarisha ndugu na dada zetu nchini Urusi na Crimea wanapoendelea kustahimili kwa ajili ya jina lake.​—Ufunuo 2:3.